1. Maana ya Hisa

Sheria ya Ushirika na. 6 ya mwaka 2013 kupitia kifungu cha 41 inatambua uwepo wa Mwanachama (member) na Mteja (client), ikiwa mwanachama ni yule aliyenunua hisa ndani ya chama wakati mteja ni yule anayetumia huduma za akiba na amana ndani ya Chama.

Hisa ni uwekezaji wa msingi kabisa kwa Mwanachama. Hisa humfanya mwanachama kuwa mmilikia halali wa SACCOS.

2. Aina za Hisa

Kuna aina mbili za hisa ambazo mwanachama anaweza kuchangia ambazo ni;

  • Hisa za lazima
  • Hisa za ziada

Hisa za lazima ndiyo hisa za umiliki wa Chama, ni kiwango cha chini cha hisa ambazo kila mwanachama anatakiwa kumiliki ndani ya Chama. Hadi sasa hisa za msingi kwa HAZINA SACCOS Ltd ni kama ifuatavyo;

-Kiwango cha cha chini cha idadi ya Hisa ni 25

-Thamani ya kila hisa ni Tsh. 20,000/=

-Hivyo, kiwango cha chini cha thamani ya hisa kwa kila mwanachama ni Tsh. 500,000/=

Hisa za ziada ni zile ambazo mwanachama atachangia juu ya hisa za msingi. Aidha mwanachama anaweza kuchangia hisa za ziada mpaka 20% ya Hisa zote za Chama(Hazina Saccos Limited).