Mkopo wa Dharura 1
 Kiwango cha juu cha mkopo huu ni Tsh 5,000,000/= na kutoza riba 1.5% kwa mwezi. Muda wa juu wa marejesho ni miezi 12, mkopo huu hutolewa ndani ya masaa 24 baada ya kukamilisha taratibu za maombi.

Mkopo wa Dharura 2
Kiwango cha juu cha mkopo huu ni Tsh 10,000,000/= na kutoza riba 1.5% kwa mwezi. Muda wa juu wa marejesho ni miezi 24, mkopo huu hutolewa ndani ya siku saba (07) baada ya kukamilisha taratibu za maombi.

Mkopo wa Tuliza Moyo
 Kiwango cha  mkopo huu ni kuanzia Tsh 300,000/= hadi Tsh.1,000,000  bila riba. Muda wa marejesho ni siku 30, mkopo huu hutolewa ndani ya masaa 24 baada ya kukamilisha taratiu za maombi.

Mkopo wa Elimu
Kiwango cha juu cha mkopo huu ni Tsh 5,000,000/= na kutoza riba ya 0.42%. Muda  wa kurejesha mkopo ni miezi 24. Fomu hupokelewa kuanzia tarehe 1 – 20 ya kila mwezi.

Mkopo wa Mazishi
Kiwango cha juu cha mkopo huu ni 3,000,000/= na kutoza riba ya 0.42% . Muda wa kurejesha mkopo huu ni miezi 24 , mkopo huu hutolewa pale mwanachama anapokuwa amefiwa baba,mama, mtoto, mume au mke.

 Mkopo wa sikukuuu
Kiwango cha juu cha mkopo huu ni 500,000/= na kutoza riba ya 0.84%. Muda wa juu wa kurejesha mkopo ni miezi 6. Hutolewa kwa sikukuu za Krismas, Pasaka, na Idd  El-fitri

Mkopo wa Maendeleo
Kiwango cha juu cha mkopo huu ni mara tatu (3) ya akiba za mwanachama na kutoza riba ya 0.84%. Muda wa kurejesha mkopo huu ni miezi 12 – 60. Hutolewa mwishoni mwa mwezi na fomu hupokelewa kuanzia tarehe 1-20 ya kila mwezi.

Mkopo wa Biashara
Kiwango cha juu cha mkopo huu ni mara tatu (3) ya akiba za mwanachama na kutoza riba ya 0.84% kwa mwezi. Muda wa kurejesha mkopo huu ni miezi 12 – 60. Fomu hupokelewa kuanzia tarehe 1-20 ya kila mwezi.

Mkopo wa Ujenzi
Kiwango cha juu cha mkopo huu ni mara tatu (3) ya akiba za mwanachama na kutoza riba ya 0.84% kwa mwezi. Muda wa kurejesha mkopo huu ni miezi 12 – 60. Fomu hupokelewa kuanzia tarehe 1-20 ya kila mwezi.

 Mkopo wa utaratibu wa Bank (Standing Order)
Kiwango cha juu ni Tsh 20,000,000.00 na kutoza riba ya 1.5%. Muda wa kurejesha ni miezi 36. Fomu hupokelewa kuanzia tarehe 1-20 ya kila mwezi.

Mkopo wa Viwanja
Hutegemea na taratibu zitakazowekwa na chama kwa wakati huo.