1.Utangulizi

Amana ni fedha anayoiweka mwanachama kwa lengo la kujiwekea akiba inayoweza kumsaidia badae. Amana ni fedha inaweza kuwekwa muda wowote na kutolewa ama kupunguzwa muda wowote.

    2.Aina ya Amana

Ili kuendesha Chama kibiashara, Hazina  SACCOS Ltd imeweka makundi 2 makuu ya aina za amana ambayo ni;-

  • Amana ya Kawaida
  • Amana ya Muda Maalum

Amana ya kawaida ni fedha anayoiweka mwanachama muda wowote na anaweza kuitoa muda wowote anapohitaji isipokuwa kama kiwango kinachotolewa ni kikubwa kuliko kiwango kilichoainishwa kwenye Masharti Mwanachama atatakiwa kutoa notisi ya siku 7.

Kwa upande mwingine amana ya muda maalum ni amana ambayo Mwanachama aningia makubaliano au mkataba na Chama kutoichukua amana yake kwa muda uliokubaliwa kwa ahadi ya Chama kumlipa riba ndani ya kipindi cha makubaliano. Viwango vya riba katika amana ya muda maalum vitatokana na hali ya biashara pamoja na viwango vya soko la fedha.

  3. Taratibu za Uwekaji Amana

Chama kina fomu maalum kwa ajili ya Mwanachama kujaza na kuweka amana. Kuna fomu tofauti za Amana ya kawaida na amana ya muda maalum.