
MWELEKEOWACHAMA
Mafanikio
Chama cha HAZINA SACCOS LTD katika utoaji wa Huduma kwa wanachama umepata mafanikio yafuatayo:
1. Hadi sasamwezi wa nane 2012 chama kinaidadi ya wanachama 1575
2. Chama kimeweza kutoa mikopo maalum,maendeleo,dharura,elimu na sikukuu
3. Chama kina ofisi za Huduma katika jengo la PAT lililoko Wizara ya Fedha
4. Chama kimefanikiwa kuajiri wafanyakazi sita ambao wako ofisini muda wote(full time)
5. Chama kimefanikiwa kukamilisha na Kuwasilisha Hesabu za chama zilizokaguliwa (audited accounts) kwa mujibu wa sheria.
Matarajio
Katika kipindi cha miaka kumi (10) ijayo chama cha HAZINA SACCOS kinatarajia:
Kupanua uwigo wa wanachama kwa kuwakaribisha wafanyakazi wa taasisi mbalimbali za serikali.
Kuanzisha Huduma za Kibenki (FICOS) kwa wanachama wake kwa siku zijazo.
Kuongeza Idadi ya wafanyakazi na matawi ya Huduma ili kusogeza Huduma za mikopo kwa wanachama.
Kutoa mafunzo kwa wafanyakazi ili kuongeza ufanisi wa kazi na kuweza kukabiliana na mabadiliko ya uchumi, sayansi na teknolojia nchini na ulimwenguni kwa ujumla wake.
Kutoa Elimu ya Ushirika na Ujasiliamali kwa wanachama ili kuongeza tija kwa shughuli zao.
Kufungua miradi mbalimabali ya chama kwa ajili ya maendeleo ya chama.