• +255 683 865 660
  • This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.
  • Mon-Fr 8:00 Am - 15:00 Pm

About Us

About Us

Image

About Hazina Saccos Ltd


HAZINA SACCOS ni nini?
Ni Ushirika wa Akiba na Mikopo kwa ajili ya kuinua, kustawisha na kuboresha hali za wanachama wake.

Historia
Ushirika huu ulianzishwa mwaka 1972 na kusajiliwa rasmi tarehe 21/03/1973 na wanachama wasiopungua 250 hadi sasa kuna jumla ya wanachama 1275.

Maono (vision):
Ni kuwezesha kukua Ushirika wa Akiba na Mikopo unaotoa huduma za fedha ambazo ni bora, nafuu,rahisi,zinazokidhi na kuridhisha kwa wanachama.

Lengo kuu (General Objective)
Ni kukuza ushirika wenye uwezo wa kujiendesha kwa kulipa gharama zake kukidhi mahitaji ya huduma ya kifedha ya wanachama bila kutegemea asasi/mamlaka/ watu wengine na kutoa msukumo wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii na kuwa sehemu ya mtandao wa huduma za kifedha katika misingi, njia na taratibu za Ushirika.

Malengo Mahsusi (Specific Obejectives):

·         Kuweza kukuza na kuendeleza huduma endelevu za kifedha kushiriki na kuhamasisha na kuhimiza uwekezaji wa Akiba, utunzaji salama na uhakika wa Akiba na Hisa.
·         Kuweza kujiendelesha kwa faida ili kujiimarisha na hatimaye kujitegemea kifedha na kujitosheleza kiuchumi.
·         Kuweza kutoa bidhaa mbalimbali za mikopo zifaazo kwa wanachama.
·         Kuweza kutoa Elimu ya UJASILIAMALI kwa wanachama.

© 2021 Hazina saccos ltd | All Rights Reserved | Designed by INCOMTECH technology & Consultancy | +255 714 542 375 | +255 717 790 830